Uncategorized

KMC YACHEKELEA KUTUPWA RWANDA KIMATAIFA

admin July 24, 2019 1:31 am


UONGOZI wa KMC umesema kuwa ushiriki wao wa michuano ya Kagame umewajenga hivyo wamepata uzoefu wa kutosha kwenye michuano ya kimataifa.

KMC ilialikwa kwenye michuano ya Kagame iliyofanyika nchini Rwanda na kwenye micuano ya kimataifa mchezo wao wa kwanza watacheza na AS Kigali ya Rwanda.

Ofisa Habari wa KMC, Anwari Binde amesema lazima wawatoe kimasmaso watanzania kwa kufanya maajabu.

“Uzoefu tulioupata kwenye michuano ya Kagame ukizingatia kwamba tumeifunga Rayon Sports ambao ni mabingwa watatufanya tuamini kwamba tuna kikosi imara  hivyo tunakwenda kupambana,” amesema.

KMC itamenyana na AS Kigali kati ya Agosti 9/11 mchezo wa kombe la Shirikisho nchini Rwanda kabla ya kurudiana Agosti 23 au 25 Dar.

MANCHESTER CITY: HATUJAPATA OFA YA BAYERN MUNICH KUMTAKA SANE LIVERPOOL: TUNAJIPANGA KWA AJILI YA MSIMU UJAO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply