![]() |
DK MWAKYEMBE |
Baada ya mzunguko, hatimaye Waziri Mkuu wa Habari, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe amewataka viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF kuongeza uwazi katika masuala mbalimbali ili waweze kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuondoa Hali ya sintofahamu ambayo inaweza kujitokeza.
Mwakwembe ameeleza hayo baada ya kikao walichokifanya juzi Julai 23 na 24 na viongozi wa TFF, BMT, Bodi ya ligi, TRA na viongozi wa masoko ambao walijadili juu ya suala michuano ya Afcon na kile kilichotokea baina yake na viongozi wa TFF kufuatia kutofanyika kwa mkutano wa awali.
Mwakyembe amesema kuwa, wamefungua ukurasa mpya na TFF kutokana na mkutano walioufanya siku mbili mfululizo ambapo amepata majibu ya Yale ambayo alikuwa akiyahitaji ambapo tayari TFF wameshamkabidhi ripoti ya Afcon ambapo amewataka viongozi hao kuwa wawazi kwa Serikali na kwa wakati ili kuweza kusaodiana.
“Nimefanya kikao mfululizo na viongozi wa TFF, Bodi ya Ligi, BMT na TRA tumejadili vitu vingi likiwemo suala la mashindano ya Afcon yaliyomalizika, tumejadiliana na sababu zote wameweka mezani, awali kulionekana kuna mvutano lakini ilikuwa suala la kuwekana wazi.
“Mimi nilizungumza na Amunike alinieleza kilichotokea pia baadhi ya wachezaji tulizongumza lakini baadhi ya vyombo vya habari vililipoti kuwa mimi nampenda Amunike si kweli.
“Serikari kazi yake kusimamia na wenye maamuzi ni TFF , nashukuru nimeipata ripoti ya Afcon kikubwa kinachotakiwa kati yetu ni ushirikiano.
“TFF inatakiwa iongeze uwazi kwa Serikali na kwa wakati ili Selekari iweze kutoa mchango wake kwa wakati hivyo tumekubaliana kufungua ukurasa mpya kuanzia leo.
Aidha vitu vingine alivyojadili ni pamoja na:
Kurekebisha kanuni ya uwekezaji:
” Tumejadiliana vitu vingi katika kikao hicho ikiwemo suala zima la uwekezaji katika klabu zilizoanzishwa na jamii ikiwemo Simba, Yanga, Coastal Union na timu nyinginezo, nimeagiza Baraza la Michezo kurekebisha kanuni ya uwekezaji ili kuendana na nchi za wenzetu kupata mwekezaji zaidi ya mmoja katika timu kwani nchi nyingine mwekezaji anakuwa zaidi ya mmoja tofauti na hii ya kwetu. imekuwa tatizo katika mgawanyiko wa mali katika hili asilimia 49 ya mwekezaji na 51ya wanachama.
“Suala hilo litabaki BMT nitaunda kamati ndogo ambayo itashirikisha wajumbe wachache kutoka BMT, TFF, wadau wa michezo na TRA ambao ndio watakaohusika na ubadilishaji wa kanuni.
Suala la wachezaji wa kigeni;
“Suala lingine ambalo tumelizungumzia ni kuhusu idadi ya wachezaji wa kigeni, wamelifafanua kuwa adhima ilikuwa kufufua soka letu, tumeona Simba na Yanga wametusaidia sana tuna timu nne zitakazoshiriki kimataifa, pia imesaidia idadi ya mawakala kuongezeka hapa nchini.
” Nimefurahi nilivyoelezwa kuwa wachezaji wa kimataifa wakija wanalipa ada ni Jambo zuri pia masharti ya wachezaji wote wa kigeni kucheza timu za taifa na ligi inayoeleweka imepunguza kuwa na ifadi kubwa ya wachezaji .
Klabu ligi kuu kuwapa nafasi wachezaji vijana;
“Tumekubaluana klabu zote za ligi kuu zisajili wachezaji watatu kutoka timu zao za vijana U-20 na wawape nafasi ya kucheza katika kila mechi wasiwaweke benchi