Home Uncategorized KOCHA YANGA ATAJA SIKU YA KURUDI BONGO

KOCHA YANGA ATAJA SIKU YA KURUDI BONGO

MWINYI Zahera Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa ameskia juu ya suala la wachezaji wake kugoma kujiunga na kambi kwa kutolipwa mshahara pamoja na yeye kugomea kurejea Bongo jambo ambalo halina ukweli.

Zahera bado hajajiunga na timu kambini Morogoro na amesema kuwa anarejea muda wowote kuanzia sasa.

“Naskia kwamba naidai timu ya Yanga, hakuna ukweli siidai hata elfu moja timu ya Yanga na kwa sasa nipo likizo nikimaliza likizo yangu nitarejea muda wowote kuanzia sasa,” amesema.

Yanga imeweka kambi Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao na inafanya kazi chini ya kocha msaidizi Noel Mwandila.

SOMA NA HII  MTAMBO WA MABAO YANGA WAFICHUA MAANA YA KUSHANGILIA KWAKE