Uncategorized

SIMBA MSIMU UJAO MCHEZAJI MMOJA KUCHEZA ZAIDI YA NAFASI MOJA, MIFUMO MPAKA MITATU

admin July 26, 2019 4:36 pm


PATRICK Aussems,Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa anataka kuona wachezaji wake wanacheza nafasi zaidi ya moja ili kutumia mifumo miwili au mitatu msimu ujao.

 Msimu uliopita, Aussems alitumia mifumo miwili zaidi, ule wa 3-5-2 hasa kipindi Shomari Kapombe akiwa fiti lakini baadaye alitumia zaidi ule mfumo wa 4-4-2.
Simba inajiaanda na michuano ya kimataifa ambapo mchezo wa kwanza utakuwa kati ya Agosti 9-11, mwaka huu
kabla ya ligi kuanza dhidi ya UD Songo ya Msumbiji, ikianzia ugenini.
Aussems amesema: “Nataka kuona wachezaji wangu wakicheza nafasi zaidi ya moja, sababu msimu ujao nataka kuwa na mifumo miwili au mitatu.
Simba katika maandalizi yake hayo imefanikiwa kucheza mechi mbili ambazo ni dhidi ya Platinums Stars (ilishinda mabao 4-1) huku ikicheza na Orbret TVET na kushinda 4-0.

MBEYA CITY: KAZI KUBWA ITAFANYIKA MSIMU UJAO ARSENAL WABISHI KINOMA WAKOMAA NA AUBAMEYANG

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply