Home Uncategorized KIPA STARS ATAMBA KUWAZUIA WASHAMBULIAJI WA KENYA

KIPA STARS ATAMBA KUWAZUIA WASHAMBULIAJI WA KENYA

JUMA Kaseja ametamba kuwazuia washambuliaji wa timu ya taifa ya Kenya kwenye mechi ya kufuzu michuano ya CHAN itakayopigwa kesho, Julai 28 Uwanja wa Taifa, Dar.
Kaseja mara ya mwisho kuitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ilikuwa mwaka 2013, amesema  anaamini anaweza kufanya mambo makubwa.
“Kwa sasa nina majukumu na timu ya taifa na jukumu lenyewe ni kuhakikisha nalisaidia taifa langu katika mchezo dhidi ya Kenya, hilo siku zote ni jukumu la kila mchezaji kuhakikikisha analisaidia taifa lake.
“Naamini kuwa tutafanya vizuri kwenye mchezo wetu kwa kuwa wote tupo kwenye morali ya juu,” amesema.

Kaseja anaungana na mlinda mlango Metacha Mnata wa Yanga na Aishi Manula wa Simba na yeye anakipiga KMC kwa sasa.
SOMA NA HII  KOCHA KAGERA SUGAR AWATAKA WACHEZAJI WASIPUUZIE MAZOEZI