Uncategorized

SIMBA YAWEKA MEZANI MILIONI 10 KWA AJILI YA KELVIN YONDAN, METACHA MNATA, JUMA KASEJA

admin July 28, 2019 1:35 am


UONGOZI wa Simba umesema kuwa endapo timu ya Taifa ya Tanzania itaibuka kidedea mbele ya timu ya Kenya leo watapewa zawadi ya milioni 10.

Zawadi hizo zitakuwa ni kwa timu nzima kwa ajili ya pongezi ambayo imelenga kuwapa morali wachezaji hao ili kupata matokeo chanya kwenye mchezo wa leo wa kufuzu Chan utakaochezwa uwanja wa Taifa.

Kupita kwenye ukurasa wa Instagram wa Simba taarifa iliandikwa kuwa ahadi hiyo imetolewa na Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori kwa niaba ya Simba.

Miongoni mwa wachezaji wa timu ya Taifa ni pamoja na Kelvin Yondan, Metacha Mnata, Paul Godfrey, Aish Manula, Juma Kaseja, Erasto Nyoni na Ibrahim Ajib ambao mkwanja huo wa milioni 10 unawahusu.

JUMA BALINYA, SIBOMANA NA KIPA WA KENYA KUTOA ZAWADI YA NGUVU LEO MOROGORO SEPETU: WACHEZAJI WALITUANGUSHA AFCON, LEO HAPANA, MASHABIKI TUJITOKEZE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply