Uncategorized

HIMID MAO ACHEKELEA CHANGAMOTO MPYA NDANI YA MISRI

admin July 31, 2019 6:23 am

HIMID Mao amesema kuwa ana furaha kwa sasa kuanza changamoto mpya ndani ya kikosi cha ENNPI kwa kandarasi ya miaka miwili.


Mao ambaye ni nahodha msaidizi wa kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania amesaini kandarasi hiyo akitokea klabu ya Petro Jet FC ya nchini Misri na kandarasi yake hiyo mpya ina kipengele cha kuongeza mkataba mpya.

Ndani ya Petrojet FC Mao alicheza michezo 32 na kupachika nyavuni jumla ya mabao matatu.

“Nina furaha kuwa ndani ya klabu mpya kwa sasa ambayo ni Enppi ninachokitazama kwa sasa ni mafanikio makubwa.

“Asante wachezaji wenzangu wa klabu ya Petrojet FC, benchi la ufundi pamoja na mashabiki kwa sapoti yenu na ninawatakia kila la kheri acha nipambane na changamoto mpya,” amesema.
SIMBA: TUMEFUNGA HESABU KISHUJAA AFRIKA KUSINI KAMBI YA SIMBA YAVUNJWA AFRIKA KUSINI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply