Uncategorized

SIMBA: TUMEFUNGA HESABU KISHUJAA AFRIKA KUSINI

admin July 31, 2019 6:13 am


PATRICK Aussems, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa uwezo wa wachezaji wake umeimarika hivyo ana imani kubwa watakuwa na kitu cha kipekee msimu ujao.

Simba jana ilifunga hesabu nchini Afrika Kusini kwa kutoka sare ya kufungana bao 1-1 na Orlando Pirates mchezo wa kirafiki uliochezwa Afrika Kusini.

Aussemss amesema:-“Tumemaliza kambi na Orlando Pirates ambao wapo tayari kuliko sisi wao wametumia muda mwingi kujiaandaa kwa ajili ya msimu ujao tofauti na sisi.

“Napenda kuwapongeza wachezaji wangu tulikuwa na wakati mzuri sana Rustenburg, kila mmoja kafanya kazi nzuri tunaweza kusema hii kambi imekuwa nzuri sana na nimeridhishwa kwa hatua ambayo tumefika,” amesema.

HUYU NDIYE MWILI JUMBA ALIYESHUSHWA NA YANGA KUCHUKUA NAFASI YA MAKAMBO HIMID MAO ACHEKELEA CHANGAMOTO MPYA NDANI YA MISRI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply