Home Uncategorized KOCHA MPYA YANGA AANZA KAZI NA KINDOKI

KOCHA MPYA YANGA AANZA KAZI NA KINDOKI


KOCHA wa makipa ndani ya Yanga, Peter Manyika amesema kuwa ameanza kazi na mlinda mlango Klaus Kindoki ambaye msimu uliopita mashabiki hawakumkubali kutokana na kufanya makosa mengi ya kiufundi.

Moja ya mechi ambayo Kindoki alifanya makosa ya kiufundi ni kwenye mchezo wake wa kwanza dhidi ya Stand United ambapo aliruhusu kufungwa mabao 3 na Alex Kitenge licha ya Yanga kushinda kwa mabao 4-3.

Akizungumza na Saleh Jembe, Manyika amesema kuwa ameangalia namna bora itakayomfanya awe katika ubora wake msimu ujao.

“Nimeanza na kuangalia namna bora ya kumrejesha kwenye ubora wake mlinda mlango Kindoki, msimu uliopita alifanya makosa mengi ya kiufundi hicho ndicho tunachokifanyia kazi, nina imani kwa programu ambayo wataifanya mambo yatakuwa safi,” amesema.

Manyika amechukua nafasi ya Juma Pondamali ambaye amesema kuwa kwa sasa anataka kufanya kazi nyingine mbali na mpira.

SOMA NA HII  YANGA WAPEWA ONYO MAPEMA KABISA BAADA YA KUSHINDA