Home Uncategorized KOCHA STARS:TUNAKWENDA KUPINDUA MEZA KIBABE KENYA

KOCHA STARS:TUNAKWENDA KUPINDUA MEZA KIBABE KENYA

ETTIENE Ndayiragije Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ amesema kuwa sare waliyoipata sio mbaya wanakwenda kupindua meza nchini Kenya.

Stras ililazimisha sare ya bila kufungana na timu ya Taifa ya Kenya kwenye mchezo wa kwanza wa kutafuta tiketi ya kushiriki michuano ya Chan uliochezwa uwanja wa Taifa.

Ndayiragije amesema:”Perfomance yetu ilikuwa nzuri licha ya kushindwa kupata matokeo ila kikubwa ni kwamba wachezaji walikuwa bado hawajazoeana awali ni kazi kubwa ambayo kwa sasa tunaifanya.

“Hatujaruhusu bao ni kitu chanya hivyo hatuna presha  ya kulazimisha sare mchezo wa marudio, makosa ya kushindwa kumaliza nafasi tulizozitengeneza tayari tumeanza kuyafanyia kazi hivyo tunakwenda kutafuta matokeo chanya.

“Wachezaji wetu wameshaanza kuzoeana tofauti na mwanzo walikuwa bado wageni ila wamepambana kwa hali na mali,” amesema.

Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Agosti 4 nchini Kenya na ili kufuzu michuano hii ni lazima Stars ishinde.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA ALHAMISI