Uncategorized

NEYMAR PASUA KICHWA NDANI YA PSG

admin August 2, 2019 8:52 am


NEYMAR Jr, amewaambia mabosi zake wa Paris Saint-Germain (PSG) kuwa hawezi kucheza ndani ya kikosi hicho kwa sasa.

Ripoti zinaeleza kuwa huo ni mpango wa Neymar kutoa shinikizo Kwa PSG wampe ruhusa ya kutimkia Barcelona.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 ambaye ni nyota pia ndani ya kikosi cha timu ya Taifa ya Brazil hesabu zake Kwa sasa ni kurejea Nou Camp.

 
Mabosi wa PSG wanahitaji dau la pauni milioni 273 ili kumrejesha nyota huyo ndani ya Barcelona.

Ripoti zinaeleza kuwa Neymar amesema Kwa sasa haitaji kujiunga na PSG na hayupo tayari kuendelea kuwa ndani ya kikosi hicho.

Mpaka sasa Neymar hajacheza mchezo wowote ndani ya PSG baada ya kurudi ndani ya kikosi hicho msimu huu.

MATOLA: MASHABIKI WAIPE SAPOTI STARS, NAFASI BADO IPO KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA BOTSWANA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply