Uncategorized

YANGA: NUNUENI JEZI HALISI KWA MANUFAA YA KLABU, UBORA WAKE HAKUNA MFANO BONGO

admin August 2, 2019 12:32 pm


MSHINDO Msolla, mwenyekiti wa Yanga amesema kuwa mashabiki wa Yanga wanunue kwa wingi jezi halisi ambazo zimezinduliwa leo kwa manufaa ya klabu.

Msolla amesema:”Wakati nazunguka kwenye matawi mashabiki na wanachama walikua wananiambia hawataki kununua jezi kwasababu club hainufaiki. Sasa nawambia wanunue kwa sababu club inanufaika.

“Hakikisha unanunua jezi halisi. Tayari zimeanza kuuzwa kwenye maduka ya GSM Msasani Mall, Pugu Mall na makao makuu ya Yanga.


Nayo waliotengeza jezi hizo kampuni ya GSM kupitia mwakilishi wao wamesema:-
“Hakuna jezi yenye ubora kama huu tutakao zindua leo nchini Tanzania. Pia tutafungua duka kubwa la vifaa mbalimbali vyenye nembo ya Yanga.Hamjawahi kuona duka la Kimataifa kama hilo.”

IDRSSA GUEYE: ULIKUWA MPANGO WANGU KUTUA PSG, NINA FURAHA KWA SASA SIMBA WAPEWA MAMILIONI YA KUTOSHA NA SportPesa

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply