Home Uncategorized DAU LA SAMATTA NOMA, GENK WAZIDI KUMKOMALIA KINOMA

DAU LA SAMATTA NOMA, GENK WAZIDI KUMKOMALIA KINOMA


UONGOZI wa klabu ya KRC Genk umeamua kuongeza tena dau kwa timu zinazomtaka mshambuliaji wake, Mtanzania Mbwana Samatta kutoka shilingi bilioni 40 hadi kufikia bilioni 53.

 Mshambuliaji huyo msimu uliopita alifunga mabao 23, katika Ligi Kuu ya Ubelgiji, amekuwa akitakiwa na timu nyingi za England zikiwemo Leicester, Middlesbrough na Aston Villa lakini wapo Galatasaray ya Uturuki.
Taarifa za uhakika kutoka nchini Ubelgiji, zinaeleza Genk wameamua kuongeza dau tena kwa mshambuliaji huyo kwa lengo la kutaka kubaki naye baada ya Galatasaray kuongeza fedha tena kutoka bilioni 26 hadi kufikia bilioni 40.
Inadaiwa Genk wamekuwa wagumu kumuachia Samatta kwa kuwa wanamhitaji kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hali ambayo imekuwa ikiwapa ugumu Galatasaray kumalizana nao licha ya Leicester na Aston Villa kuendelea kusubiri mwishoni.
“Suala la Samatta kuondoka sasa limeanza kubadilika kutokana na ugumu ambao umeanza kujitokeza baada ya Genk kuamua kuongeza dau la mchezaji husika kutoka lile la awali ingawa Galatasaray wameamua kukomaa kufuatia kuongeza pesa yao na kufikia bilioni 40.
“Kikubwa kinachoonekana kwa Genk ni kwamba hawataki kumuachia kwa ajili ya michuano ya UEFA ndiyo maana wamekuwa wakipandisha dau kila wakati ingawa Galatasaray ndiyo wamebaki kwenye meza ya mazungumzo hadi sasa na hao wengine wanasubiri kama kutakuwa na mabadiliko yoyote,” kilisema chanzo.
SOMA NA HII  ISHU YA AJIBU KUFELI TP MAZEMBE YAVUJA