Uncategorized

NYOSSO KUKIPIGA NDANI YA RUVU SHOOTING

admin September 1, 2020 2:47 pm

 


JUMA Nyosso, mkongwe ndani ya Ligi Kuu Bara msimu ujao atakipiga ndani ya Klabu ya Ruvu Shooting inayonolewa na Kocha Mkuu, Charles Boniface Mkwasa.


Nyosso alikuwa nahodha ndani ya Kagera Sugar msimu wa 2019/20 mkataba wake uliisha ndani ya timu hiyo na mabosi hawakumuongezea mkataba mpya.

Habari zinaeleza kuwa tayari kwa sasa ameshamalizana na Ruvu Shooting akiwa ni mchezaji huru.

“Nyosso kwa sasa ni mali ya Ruvu Shooting kwa kuwa mkataba wake ndani ya Kagera Sugar ulikwisha hivyo ameingia ndani akiwa ni mchezaji huru na ataendelea kuwa ndani ya ligi msimu wa 2020/21.” alisema mtu wake wa karibu.

 

NYOTA YANGA ASAINI POLISI TANZANIA BEKI GABRIEL NI MALI YA ARSENAL, ARTETA AMPA NENO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply