Uncategorized

GSM WASHUSHA MZIGO WA JEZI MPYA ZA YANGA…

admin August 5, 2019 1:36 pm



Kampuni ya GSM leo wameshusha mzigo mpya wa jezi za Yanga nchini baada ya hule wa awali kumalizika saa chache mara baada ya kuzinduliwa.


Akizungumza na Waandishi wa Habari, Kaimu Katibu wa Yanga, Dismas Ten alisema kuwa mzigo huo mpya wa jezi unapatikana kwenye Mail zote za GSM za Pugu na Msasani.


Ten alisema kuwa, ni nafasi pekee ya mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kununua jezi hizo tayari kwa ajili ya kwenda kuisapoti itakapokuwa Uwanjani Jumapili hii ikicheza na Township Rollers ya Botswana.


“Nichukue nafasi hii kuwatangazia mashabiki wa Yanga kuwa jezi mpya za timu yao tayari zipo madukani zitakazopatikana kwenye GSM Mail zote za hapa jijini Dar es Salaam,”alisema Ten.

BAADA YA WIKI YA WANANCHI, YANGA KUPAA ZANZIBAR KESHO KUMEKUCHA, YANGA YACHARUKA, YAISHITAKI SELCOM KWA SERIKALI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply