Uncategorized

SIMBA: TUTAKACHOFANYA SISI WAPINZANI WETU YANGA HAWAJAKIFANYA NA NI NOMA LEO

admin August 6, 2019 7:36 am


UONGOZI wa Simba umesema kuwa leo hakuna namna yoyote jambo la kwanza ni mashabiki kujaza uwanja kisha burudani zitafuata.

Haji Manara Ofisa Habari wa Simba amesema:”Tunajua kwamba wenzetu wamefanya kitu kizuri ila sisi ni hatua nyingine hasa kwa ubunifu na ubora wa kile ambacho tunakifanya mwanzo mwisho. 

“Kila kitu kipo kwenye mpangilio bora na staili ambazo zitatumika kwenye utambulisho wa wachezaji haijawahi kutokea tangu kuumbwa kwa nchi.

 “Hapa ni chuo cha ubunifu hivyo nawaambia mashabiki wa Simba wajitokeze kwa wingi Uwanja wa Taifa kushuhudia namna tutakavyofanya,” amesema.

Simba leo inahitimisha kilele cha SportPesa Simba wiki ambapo watacheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa na timu ya Power Dynamo.

AZAM FC: TUNAFANYIA KAZI MAPUNGUFU YETU KWA MICHUANO YA KIMATAIFA KMC YAONYOOSHA MABAO 2-1 KARIOBANG SHARK

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply