Uncategorized

MRITHI WA MAKAMBO YANGA ATABIRIWA MAKUBWA , HIKI NDICHO KINACHOMPONZA ASHINDWE KUTAMBA

admin August 12, 2019 12:39 pm

MWINYI Zahera, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wale ambao wanabeza uwezo wa mshambuliaji wake mpya, David Molinga watamuelewa tu ligi ikianza.
Molinga ni mshambuliaji mpya wa Yanga ambaye amejiunga kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea AC Lega ya Congo kuchukua mikoba ya Heritier Makambo ambaye ametimkia AC Horoya.

Zahera amesema kuwa, wengi wanabeza uwezo wake kutokana na kuona hafungi mabao ila siku moja watamuelewa tu.
“Alikuwepo Makambo, walimsema baadaye wao wakakaa kimya kwa majibu yake uwanjani, hivyo kwa sasa ni zamu ya Molinga kuwaonyesha kile alichonacho.
“Kwa sasa anashindwa kuonyesha makeke kutokana na ukweli kwamba yeye alichelewa kuungana na wachezaji kwenye maandalizi ya awali, ila nina uhakika na kile alichonacho watamuelewa tu,” amesema.
TANZANITE KUREJEA LEO BONGO NA KOMBE LAO LA COSAFA SIMBA YAJIPA ANGALIZO KUELEKEA MCHEZO WA KIMATAIFA DHIDI YA UD SONGO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply