JUMA Pondamali, aliyekuwa kocha wa makipa ndani ya Yanga amesema kuwa kwa sasa atapambana na muziki kuufikisha hatua za kimataifa.
Pondamali kwa sasa amekacha kazi ya mpira na badala yake amegeukia muziki akiwa ni msimamizi, mwandishi na mwimbaji.
Akizungumza na Saleh Jembe, Pondamali amesema kuwa amefanya uchunguzi wa kutosha na kuona kwamba muziki una nafasi kubwa ya kumtoa kwenye maisha.
“Naifanya hii kazi haimanishi nimeanza leo nimeanza muda mrefu sana na nimetunga nyimbo nyingi za Yanga ambazo hazikupata umaarufu mkubwa kutokana na kutokuwepo na matamasha kama ambavyo wapinzani wetu walikuwa wanafanya.
“Muziki ambao nasimamia na kufanya ni Singile huku ndiko ambako nitafiti hivyo mipango mingi inakuja na nyimbo kali zinakuja, lengo kubwa ni kuvuka hatua ya kitaifa mpaka kimataifa” amesema.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.