Home Uncategorized WACHEZAJI WAWILI YANGA WABADILI UKUTA

WACHEZAJI WAWILI YANGA WABADILI UKUTA


BEKI wa pembeni wa Yanga, Paul Godfrey ‘Boxer’ ana hatihati ya kuukosa mchezo wa marudiano dhidi ya Township Rollers, lakini taarifa ziwafi kie mashabiki wa timu hiyo kuwa Kocha Mkuu Mkongomani, Mwinyi Zahera haraka ameanza kumtengeneza Juma Abdul.

Abdul tayari yupo kambini akijiandaa na mchezo huo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa huko Gaborone, Botswana baada ya ule wa awali kutoka sare ya bao 1-1 uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Beki huyo amerejea kikosini baada ya kulipwa stahiki zake alizokuwa anadai katika fedha za usajili ambazo zinadaiwa kufi kia Shilingi Milioni 40.

Zahera alisema beki huyo amemtenganisha na wenzake katika kujiandaa na mchezo huo huku akipewa programu maalum ya binafsi ya kujifua.

Zahera alisema kuwa anachokifanya hivi sasa ni kurejesha utimamu wa mwili wake kwa kumfanyisha programu ya fi tinesi katika kurejersha kasi yake ya uwanjani baada ya kukaa nje kwa muda mrefu.

“Namuandaa Abdul ili awepo katika mchezo huo wa marudiano, hivyo ameanza programu maalum ya kumuweka sawa tukiwa kambini Kilimanjaro,” alisema Zahera.

Mbali na hilo, ujio wa beki mkongwe wa Yanga, Kelvin Yondani utasababisha Zahera alazimike kumuondoa beki mmoja wa kati, kati ya Lamine Moro na Ally Sonso.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra kutoka ndani ya benchi la ufundi la timu hiyo, Zahera amepanga kumuingiza kikosini Yondani atakayecheza pamoja na Lamine huku Sonso akimpeleka pembeni kucheza namba tatu aliyokuwa anacheza Muharami Issa ‘Marcelo’.

SOMA NA HII  KAGERA SUGAR YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA YANGA