Home Uncategorized VAR INAWALIZA KINOMA MANCHESTER CITY, GABRIEL JESUS HAAMINI KABISA

VAR INAWALIZA KINOMA MANCHESTER CITY, GABRIEL JESUS HAAMINI KABISA


MENEJA wa Manchester City, Pep Guardiola amesema kuwa kuna umuhimu wa kupunguza matumizi ya teknolojia ya VAR kwani inaleta matokeo yenye maumivu.

City ililazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 na Spurs, bao la Gabriel Jesus VAR ililikataa. 


” Wachezaji wangu wanacheza kwa juhudi kutafuta matokeo mwisho wa siku wanakwama kutokana na kusubiri teknolojia iamue hii sio sawa na haileti maendeleo. 

“Jesus ni mara yake ya pili bao lake kukataliwa dhidi ya Spurs, mwezi Aprili kwenye Ligi ya Mabingwa bao lake ilielezwa ni Offside.

“Michezo ni migumu, tunajifunza kutumia mbinu mpya bado tutazidi kukazana zaidi ya hapa,” amesema.

Gabriel Jesus alitupia ujumbe kwenye twitter kuwa “Mchezo mgumu na mkubwa, tumepambana na kucheza vizuri, bahati mbaya hatujapata ushindi,” amesema na kuongeza kuwa tulifunga bao ambalo tulilihitaji lakini…


 Mabao ya Manchester City yalipachikwa dakika ya 20 na Raheem Sterling na Sergio Arguero dakika ya 35 na Yale ya Spurs yalipachikwa na Erick Lamela dakika ya 23 na Lucas Moura dakika ya 56

SOMA NA HII  KAPOMBE ABEBA MILIONI 70 SIMBA