KIKOSI cha Timu ya Taifa ya Tanzania Chini ya Miaka 15 leo kimeanza kwa kuchechemea mbele ya Uganda kwa kupoteza mchezo wa kwanza kwa kufungwa mabao 2-0.
Tanzania ambayo inashiriki michuano ya CECAFA kwa timu za Vijana chini ya Miaka 15 imepangwa kundi B na leo imetupa kete yake ya kwanza.
Michuano hiyo inafanyika nchini Eritrea uwanja wa Asmara imeanza Agosti 16 na itakamilika Agosti 30.






