BAADA ya kujiunga na Simba kwa kandarasi ya miaka miwili akitokea Yanga, aliyekuwa nahodha wa Yanga amewashukuru mashabiki na viongozi.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika ujumbe huu:-
“Hakika ilikuwa miaka miwili bora sana kwangu, ndani na nje ya uwanja, Yanga ilikua sehemu ya familia yangu.
“Nitoe shukrani zangu za dhati kwa viongozi, benchi la ufundi, wachezaji na mashabiki kwa kuniamini na kuniunga mkono katika kila jambo.
“Ni mengi nimejifunza na nina amini yatanisaidia kunijenga zaidi kama wachezaji, asante sana, hadi wakati mwingine tena, wananchi, asante,” amesema Ajibu.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.