Home Uncategorized KICHUYA AWAACHA MDOMO WAZI SIMBA

KICHUYA AWAACHA MDOMO WAZI SIMBA


Mshambuliaji wa zamani wa Simba, Shiza Ramadhan Kichuya ameibua maswali mengi kwa mashabiki wa soka nchini juu ya video aliyoweka katika mtandao wake wa Instagram.

Takribani siku saba zilizopita, Kichuya aliweka video hiyo ikimuonesha yuko Uwanja wa Ndege lakini hakuandika chochote.

Licha ya kuposti, mashabiki wake walionekana wakikomenti kutaka kujua nini safari ya wapi lakini hakutaka kujibu chochote na jitihada za kumtafuta hazikuweza kufanikiwa.

Haijajulikana ameshapata timu tayari nje ya nchi kutokana na kuwa nyumbani kwao Morogoro kwa takribani mwezi mmoja tangu amalize mkataba na timu ya Pharco iliyopo Misri kisha kupelekwa kwa mkopo ENPPI FC.

Video hiyo imewaweka njia panda haswa mashabiki wake ambao walikuwa naye bega kwa bega wakati akiichezea Simba kwani mpaka sasa hawajui ameelekea wapi au pengine ni video ya zamani.

Kichuya aliondoka Simba baada ya msimu uliopita kumalizika kutokana na kutokuwa katika mapendekezo ya Kocha, Patrick Aussems.

SOMA NA HII  BAADA YA KUIREJESHA AZAM KIMATAIFA, CHIRWA AJISOGEZA YANGA