Jezi namba 17 ambayo ilikuwa ikivaliwa na aliyekuwa mshambuliaji ya Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe ambayo sasa inavaliwa na Mnamibia, Sadney Urikhob imezua balaa ndani ya timu hiyo.
Juzi Jumatano baada ya Yanga kufungwa na Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, baadhi ya mashabiki wa timu hiyo walisikika wakilalama kuwa Sadney haitendei haki jezi hiyo ambayo ina historia na rekodi ya pekee ndani ya Yanga.
Hali hiyo ilikuja baada ya mashabiki hao kushindwa kuvutiwa na uwezo wa Sadney ambaye amekuwa akiuonyesha uwanjani tangu alipojiunga na timu hiyo akitokea Namibia huku akitajwa kama mrithi wa Tambwe katika kikosi hicho.
Kauli ya mashabiki hao kulalama imeungwa mkono na beki wa kati wa Ruvu Shooting, Rajab Zahir ambaye pia amewahi kuitumikia Yanga akisema: “Jezi hiyo hiyo ni kubwa sana kwa Sadney kutokana na rekodi yake ndani ya Yanga, hivyo anakiwa kujipanga kwelikweli.
“Msimu wa kwanza tu ambao Tambwe alitua Yanga akitokea Simba, alifanya mambo makubwa, nakumbuka mechi zake tatu tu za kwanza alifunga mabao zaidi ya sita, kumbuka alijiunga na timu katika dirisha
dogo la usajili.
“Katika mechi 13 alizoitumikia Yanga msimu huo alifanikiwa kufunga mabao 13 na kumaliza wa pili katika ufungaji nyuma ya Simon Msuva ambaye alifunga mabao 17.
“Msimu uliofuata wa 2015/16 akiwa amevalia jezi hiyo alifanikiwa kufunga mabao 21 jambo ambalo si la mchezo. “Kwahiyo Sadney ana kazi kubwa ya kufanya ili kulinda heshima ya jezi hiyo,” alisema Zahir.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.