Home Uncategorized KELVIN YONDANI AHUSISHWA SIMBA

KELVIN YONDANI AHUSISHWA SIMBA


Kocha wa Uganda aliyewahi kutamba na Simba, Jackson Mayanja anaamini kama Kelvin Yondani angekuwa kwenye ukuta wa timu hiyo asingekubali kudhalilishwa ndani ya Uwanja wa Taifa tena katika mechi muhimu kama ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mayanja amesisitiza kwamba Yondani ambaye kwa sasa anaichezea Yanga, hawezi kukubali kudhalilishwa kwa kuburuzwa kama mfungaji wa UD Songo alivyowafanyia mabeki wa Simba na kabla ya kupachika bao la aibu.

Kocha huyo ambaye hata yeye timu yake ya sasa imeondoshwa kwenye Kombe la Shirikisho aliongeza kwamba Simba ilikuwa na nafasi ya kusonga mbele ila walikosa watu makini kwenye usajili wao.

“Simba walicheza vizuri sana(dhidi ya UD Songo) hasa katika kipindi cha pili lakini tatizo walilokuwa nalo ni ukosefu wa spidi hasa katika eneo la ulinzi.

“Unaweza ukaona hata bao walilofungwa Simba, mshambuliaji mmoja anaikata difensi yote na kuingia katika boksi na kutaka kufunga bao,walichozidiwa Simba ni spidi tu wale vijana walikuwa na
uharaka wakiamua kuondoka ilikuwa ngumu kuwazuia.

“Ila walicheza vizuri sana walivyorudi kipindi cha pili sema ndiyo hivyo walikosa bahati na uharaka wa kufanya maamuzi wakiwa na mpira.

“Unajua katika ile mechi ya Simba na UD do Songo angekuwa anacheza mtu kama Yondani basi angekata watu vichwa kwa sababu wale vijana walikuwa na spidi sana hivyo asinge kubali kupitwa kirahisi vile,” anasisitiza Bosi huyo ambaye timu yake ya sasa ya KMC imeondoshwa kwenye Shirikisho na AS Kigali.

KMC VIPI?

“Kitu kikubwa kilichofanya tupoteze tukiwa nyumbani katika mchezo wa marudiano wa kombe la shirikisho dhidi ya As Kigali ni kukosa wachezaji wengi wenye kiwango na uzoefu wa kucheza mashindano ya kimataifa,”anasema Mayanja ambaye timu yake ilitolewa kwa wastani wa mabao 2-1.

“Kitu pekee kinachofanya timu yoyote ifanikiwe kwenye michuano ya Afrika ni kuwa na wachezaji bora na wenye uzoefu na kiwango cha juu cha kupambana na timu kubwa, sasa ukitizama KMC haina wachezaji hao ambao wanakiwango cha hali ya juu na huo ndiyo ukweli.

“Kwahiyo kwa levo ya wachezaji ambao nipo nao ilikuwa ngumu sana kuweza kupata matokeo mazuri ambayo yangefanya tusonge mbele katika michuano hii ya kimataifa,”anasema Kocha huyo mwenye heshima kubwa nchini Uganda.

“Wote tuliona ile mechi jinsi wachezaji walivyokuwa wanacheza utakuta beki anapita pembeni kwa nguvu lakini akipiga mpira haufi ki katika eneo sahihi ambalo lingemwezesha fowadi kufunga bao,sasa kile siyo kitu ambacho tulikubaliana wakafanye.

“Mimi niliwaambia ukweli kwamba uwezo wetu wa kucheza kombe la shirikisho au kombe la Afrika hatuna kwahiyo tulieni na tujipange na ligi.

“Kwa sababu lazima ifi ke mahali watu tuelezane ukweli kama mchezaji ulishindwa kucheza na kupata matokeo dhidi ya As Kigali utapata ushindi kwa nani, kwa sababu wale Kigali wenyewe hawana wachezaji wa levo ya kupambana kwenye mechi za kimataifa.

“Kwahiyo niliwaambia watulie kwa sababu katika yale mashindano hatukuwa na cha kupoteza na hatukuwa na kiwango bora, hivyo tujipange kwa michezo ya ligi kuu ili tuone tunafi ka wapi.

“Inabidi tuwajenge spidi tu wale vijana walikuwa na uharaka wakiamua kuondoka Kocha huyo vijana ili tupate ule ubora ambao tunahitaji kuwa nao, ili tufanye vyema katika michezo ya kimataifa kama tutapata nafasi katika msimu ujao,”anasema.

“Tutengeneze timu kwa msimu huu na tupate vijana ambao watakuwa tayari kukabiliana na timu yoyote katika mashindano makubwa.

“Kama mshambuliaji ameshindwa kumpita beki wa As Kigali,atawezaje kuwapita mabeki aina ya Pascal Wawa wa Simba, hiyo ni ngumu sana kwahiyo tutengeneze timu na tutakuwa vizuri kwa baadae,”anaongeza Kocha huyo ambaye kikosi chake kinapewa nafasi ya kuchachafya kwenye ligi ya msimu huu.

SOMA NA HII  WACHEZAJI WANAOTEMWA YANGA HAWA HAPA