Home Uncategorized RUBY AFUNGUKA KUACHANA NA MZAZI MWENZAKE

RUBY AFUNGUKA KUACHANA NA MZAZI MWENZAKE


Kuachwa au kuacha kusikie kwa wengine, usiombe yakukute! Hayo ni maneno ya mwanamuziki wa kike wa Bongo Fleva, Hellen George ‘Ruby’ ambaye juzikati zilisambaa tetesi kuwa ameachana na mzazi mwenzake, Kusah.

Ruby alisema ameamini kuna watu wako macho kuona mwenzao anaachana na mpenzi wake ili wamcheke na kumuanika kwenye mitandao ya kijamii.

“Watu wanadhani kuachana ni rahisirahisi? Kuna watu wako macho kufurahia kile watakachosikia ili wakuanike kwenye mitandao, mimi na mzazi mwenzangu bado tupo sana, watatumbua macho hadi wachoke na kwa taarifa yao tunaongeza mtoto wa pili,” alisema Ruby

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA NYUMA GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA