Uncategorized

MBUNGE SINGIDA APOKEA WAANDISHI WANAOKWENDA BURUNDI KUIPA MORALI STARS

admin September 1, 2019 9:55 am

MBUNGE wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu, ameupokea msafara wa Waandishi wa habari za michezo wanaokwenda nchini Burundi kuisapoti timu ya taifa Tanzania ‘Taifa Stars’ katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini, Qatar.

Kingu amesimamisha msafara huo katika wilaya Manyoni ambapo aliomba kupata nao chai kabla ya kuendelea na safari ya kuelekea Burundi.

Kingu amesema kuwa amefurahishwa waandishi hao kwa kuamua kwenda Burundi kuipa sapoti timu ya taifa katika mchezo huo muhimu wa kuwania kufuzu.

“Niwapongeze kwa uzalendo huu ambao mnaufanya, kiukweli siyo jambo dogo, nipo huku kwa ajili ya ziara za kijimbo ambazo huwa nafanya siku za wikiendi lakini niliposikia mnapita nikasema nitawaona, nimefurahi na hakika mnakwenda kuwa sehemu ya historia ya nchi,” alisema Kingu

DANTE HAJALIPWA MILIONI ZAKE 45 YANGA AZAM FC YAINYOOSHA TRANSIT CAMP LEO UHURU MABAO 3-1, NGOMA ALIAMSHA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply