Maduka ya wafanyabiashara wa Afrika Kusini nchini Nigeria yalivamiwa jana ikiwa ni hatua ya kujibu, mashambulizi ya hivi karibuni katika taifa hilo la Kusini mwa Afrika kufuatia wimbi jipya la chuki dhidi ya wageni.
Mashambulizi ya jana yametokea zaidi katika mji wa kibiashara wa Lagos pamoja na mji mkuu wa Abuja, na miji ya Ibadan na Uyo.
Vijana walioshikwa na hasira walichoma ofisi za kampuni ya simu ya Afrika Kusini ya MTN, na kuvamia maduka ya Shoprite.
Maduka mengine yanayomilikiwa na wafanyabiashara wa Afrika Kusini, yalikuwa chini ya ulinzi wa polisi. Maelfu ya vijana pia waliandamana katika mji mkuu wa Zambia, Lusaka dhidi ya mashambulizi ya chuki dhii ya wageni.
Umoja wa Afrika, rais wa Nigeria na mwenzake wa Afrika kusini wote wamelaani vurugu hizo.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.