Home Uncategorized MAMA WA BEKI WA YANGA KUZIKWA LEO

MAMA WA BEKI WA YANGA KUZIKWA LEO

345
0


MAZISHI ya mama mzazi wa beki wa Yanga, Juma Abdul yanatarajiwa kufanyika leo mkoani Mtwara.

Mama wa beki huyo aliyefahamika kwa jina la Rehema Abdul alifariki jana Alhamisi mkoani Mtwara na haikuwekwa wazi chanzo cha kifo chake wakati mwanae akiwa Mwanza ambapo Yanga imeweka kambi ya muda.

Uongozi wa Yanga umetoa pole kwa nyota huyo wa Yanga ambaye kwa sasa yupo kwenye kipindi kigumu na aliondoka jana Mwanza kuelekea Mtwara.