Home Uncategorized AZAM FC YAINYOOSHA TRANSIT CAMP LEO UHURU MABAO 3-1, NGOMA ALIAMSHA

AZAM FC YAINYOOSHA TRANSIT CAMP LEO UHURU MABAO 3-1, NGOMA ALIAMSHA

[the_ad id="25893"]


KIKOSI cha Azam FC, leo kimeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Transit Camp kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Uhuru.

Azam FC ilianza kupachika bao la kwanza kupitia kwa Daniel Amoah kisha Donald Ngoma alipachika jumla ya mabao mawili na lile la kufutia machozi kwa Transit Camp likipachikwa kimiani na Samson Mkwangwa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Rajabu Bwamkuu, Kocha Mkuu wa Transti Camp amesema kuwa amejifunza kutokana na makosa kwenye mchezo huo.

“Tumepoteza kwa makosa yetu ni wakati wetu kujipanga upya kwa ajili ya wakati ujao, bado ninaijenga timu na wachezaji wanajua kazi yao kushindwa sio mwisho wetu tutaendelea kupambana,” amesema. 

Trasnit Camp inashiriki Ligi Daraja la Kwanza ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 14 na imepangwa kundi B.

SOMA NA HII  AZAM FC: HATUJABAHATISHA KUTWAA FA, TULIJIPANGA KIUKWELI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here