Uongozi wa klabu ya Yanga umesema hauwezi kuelezea zaidi suala la James Kotei ambaye anatajwa kurejea Tanzania.
Taarifa zimekuwa zikisema kuwa Kotei anaweza akarejea Tanzania na awamu hii anatajwa kujiunga na mabingwa hao wa kihistoria.
Kwa mujibu wa Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz, amefunguka akieleza kuwa taarifa hizo amekuwa akiziona mtandaoni hivyo hawezi kuziweka wazi vizuri.
Aidha, Nugaz amesema kama jambo linazungumziwa inawezekana likawa lipo na akiongeza kinachotakiwa hivi sasa ni kuendelea kuwapa sapoti wachezaji waliopo.
“Naona tu kila mtu anaandika lakini siwezi kulizungumzia zaidi.
“Lisemwalo lawezekana kuja kutokea lakini nawaomba wanayanga wazidi kuwapa sapoti wachezaji waliopo.”