Home Uncategorized USHINDI WA MBAO WAMPA KIBURI SVEN, AZITOLEA MACHO POINTI TATU ZA ALLIANCE

USHINDI WA MBAO WAMPA KIBURI SVEN, AZITOLEA MACHO POINTI TATU ZA ALLIANCE

SVEN Vanderbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa ushindi mbele ya Mbao FC umewapa nguvu wachezaji wake kupambana kwenye mechi zao za ligi.

Simba kesho itamenyana na Alliance FC, Uwanja wa CCM Kirumba ikiwa na kumbukumbu ya kushinda mabao 2-1 mbele ya Mbao FC.

Sven amesema:”Wachezaji wameanza kujenga muunganiko mzuri na kwa sasa mwendo mkubwa ni kuona namna gani tutapata matokeo, mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti,” amesema.

Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 38, imecheza jumla ya mechi 15 itamenyana na Alliance iliyo nafasi ya 13 imecheza mechi 16 na pointi 20.

SOMA NA HII  CORONA YAVURUGAVURUGA MAMBO KIBAO YA ABDI BANDA