Uncategorized

AZAM FC YAFICHUA KILICHOWAPA USHINDI WA MABAO 3-1 MBELE YA FRIEND RANGERS

admin January 28, 2020 8:43 am

IDD Cheche, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa kikubwa kilichowapa ushindi mbele ya Friend Rangers ni kucheza kwa nidhamu kwa wachezaji pamoja na kufuata maelekezo.

Azam ambao ni mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho, jana Januari, 27 waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 mbele ya Friend Rangers mchezo wa hatua ya 32 bora na kwa ushindi huo wametinga hatua ya 16 bora.

“Wachezaji wanapaswa pongezi walipambana mwanzo mwisho kutafuta matokeo na walichokitaka wamekipata, kufuata maelekezo na nidhamu vimewasaidia kutimiza majukumu yao,” amesema.

Azam FC itacheza na Ihefu FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza kwenye mchezo wake wa hatua ya 16 bora.

THOMAS ULIMWENGU KUIBUKIA TP MAZEMBE GREALISH: MASHINE ASTON VILLA ITAKAYOJUMLISHA NGUVU NA SAMATTA, KUSAKA UKOMBOZI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply