Home Uncategorized KOCHA WA NAMUNGO AWAPA TANO WACHEZAJI WAKE LICHA YA KICHAPO, ISHU YA...

KOCHA WA NAMUNGO AWAPA TANO WACHEZAJI WAKE LICHA YA KICHAPO, ISHU YA BAO LA TATU AZIZUNGUMZIA NAMNA HII

HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa timu ya Namungo amesema kuwa wachezaji wake wamejitahidi kucheza mbele ya Simba licha ya kufungwa mabao 3-2.
Namungo iliyo nafasi ya tano kwenye msimamo ikiwa na pointi 28 baada ya kucheza mechi 17 ilimenyana na Simba Januari 29 Uwanja wa Taifa.
Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery amesema kuwa moja ya mpango mkubwa ilikuwa ni kupata ushindi ila kupoteza na kucheza kwa wachezaji wake anawapongeza.
“Mchezo ulikuwa mgumu, wachezaji wangu wamecheza na wanstahili pongezi, labda bao la mwisho kwangu na benchi lilikuwa na maswali mengi ila hatujui kwa kuwa maamuzi ya uwanjani yapo mikononi mwa marefa,” amesema.
SOMA NA HII  ZAHERA AJA NA RIPOTI YA BOXER YANGA, ATUMIA VIDEO KUWAFUATILIA ROLLERS