Home Uncategorized KAKOLANYA ALAMBA SHAVU SIMBA

KAKOLANYA ALAMBA SHAVU SIMBA


KOCHA wa Simba, Mbelgiji, Sven Vandenbroeck, ameonekana kuvutiwa zaidi na kiwango cha kipa Beno Kakolanya, hiyo ni baada ya kumpa shavu kipa huyo kuanza katika michezo sita kati ya 10 ambayo amekiongoza kikosi hiko tangu akabidhiwe timu hiyo mwisho mwa mwaka jana.

Katika michezo hiyo kumi, Kakolanya amewafunika makipa wenzake wa Simba, Aishi Manula aliyekuwa namba moja ambaye katika michezo kumi amefanikiwa kuanza katika michezo mitatu, huku kipa Ally Salim akifanikiwa kuanza katika mchezo mmoja pekee.

Kocha Sven alimuanzisha Beno katika mchezo dhidi ya Arusha FC katika Kombe la FA, Lipuli FC katika mchezo wa ligi, Azam FC na Mtibwa Sugar katika Kombe la Mapinduzi, dhidi ya Mbao katika mchezo wa ligi na jana Jumapili dhidi ya Alliance katika ligi.

Manula alianza katika mchezo dhidi ya KMC, Ndanda na ule wa watani wa jadi Yanga ambayo yote ikiwa ni michezo ya ligi kuu, huku kipa Ally Salim akianza katika mchezo mmoja pekee ule wa kwanza wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya Zimamoto.

Aidha, katika michezo mitano ambayo Kakolanya ameanza kabla ya jana, Simba imefanikiwa kupata ushindi katika michezo mitatu huku akipoteza mchezo mmoja dhidi ya Mtibwa kwa bao 1-0 na suluhu dhidi ya Azam michezo yote hiyo ikiwa katika Kombe la Mapinduzi.

Manula katika michezo mitatu aliyocheza amefanikiwa kuondoka na ushindi katika michezo miwili huku mmoja Simba ikitoka sare dhidi ya Yanga kwa mabao 2-2, huku Ally Salim akiipatia ushindi Simba katika mchezo mmoja alioanza dhidi ya Zimamoto.

Awali, kocha aliyeondoka hivi karibuni katika kikosi hiko, Patrick Aussems alikuwa akimtumia zaidi Manula katika kikosi cha kwanza kuliko Kakolanya ambaye alikuwa akipata nafasi ya kucheza mara chache zaidi, ambapo kwa sasa kocha Sven ameonekana kumtumia zaidi kipa Kakolanya.

SOMA NA HII  BERNARD MORRISON: SIMBA WALIKUWA NA HAKI YA KUNIFUATA

2 COMMENTS

  1. Hello,

    Wondering if you accept guest posts or link inserts on existing posts on sokalabongo.com?

    How much would you charge for this?

    Justin

    If you’d like to unsubscribe click the following link.

    https://mailerking.xyz/optout/?site=sokalabongo.com

  2. Hello Justin, we are accept guest post and per article we charge $ 350, if your so interested please reach us through email, Sokalabongo17@gmail.com for more discussion