Home Uncategorized RUVU SHOOTING YAIPIGA MKWARA MWINGINE YANGA, YATAKA MABAO MENGI KINOMA

RUVU SHOOTING YAIPIGA MKWARA MWINGINE YANGA, YATAKA MABAO MENGI KINOMA


MASAU Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting amesema kuwa wanahitaji kushinda mbele ya Yanga kwa mabao zaidi ya mawili kwa kuwa wanajiamini.

Kesho, Uwanja wa Taifa, saa 1:00 usiku, Ruvu itamenyana na Yanga ikiwa na kumbukumbu ya kuwatungua kwa bao 1-0 mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Uhuru, bao pekee la ushindi lilifungwa na Sadat Mohamed.

Bwire amesema kuwa:-“Tupo imara na tunatambua kwamba tutakutana na Yanga ambao nao wapo vizuri hilo halitupi shida, tunaendelea na kampeni yetu ya kupapasa kama ilivyo ada.

“Tumeshinda mchezo wetu kwa bao 1-0 mbele ya Mtibwa Sugar, hatujafurahi kwani ni ushindi mdogo tunapenda kushinda mabao zaidi ya mawili kwani uongozi upo pamoja nasi na wachezaji wanapambana,”.

SOMA NA HII  YANGA AMUENI, KINDOKI ANASTAHILI AONDOKE, SHIKALO NA WATANZANIA ITAWEZEKANA