Uncategorized

KINACHOIBEBA AZAM FC HIKI HAPA NDANI YA LIGI KUU BARA

admin February 12, 2020 10:55 am

IDD Cheche, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesema kuwa kikubwa kinachowapa ushindi ni wachezaji kujituma ndani ya uwanja na ushirikiano wao.

Azam FC jana ilishinda mbele ya Polisi Tanzania bao 1-0 mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Uhuru.

Akizungumza na Saleh Jembe, Cheche amesema kuwa wachezaji wanastahili pongezi na ana amini wataendelea kupambana kwenye mechi zao zote.

“Wachezaji wana juhudi uwanjani na wanastahili pongezi hicho ndicho ambacho kilicho nyuma ya ushindi wetu na mashabiki pia tunawaomba waendelee kutupa sapoti,” amesema.

Bao la ushindi kwa Azam FC lilifungwa na Mudhathir Yahaya dakika ya 49 kwa pasi ya Nicolas Wadada na kuifanya ifikishe jumla ya pointi 44.

HIVI NDIVYO YANGA ILIPOKUBALI KULAZIMISHA SARE YA KUFUNGANA BAO 1-1 NA MBEYA CITY JOHN BOCCO BALAA LAKE MBELE YA MTIBWA LILIKUWA NAMNA HII

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply