Michezo Bongo

JKT Tanzania Yaomba Radhi, Yampa Pole Pacome

Vardo July 1, 2026 10:45 am

Timu ya JKT Tanzania imeomba radhi na kumpa pole mchezaji wa Yanga, Pacome Zouzoua aliyeeshindwa kuendelea na mchezo wa Ligi Kuu baada ya kufanyiwa rafu mbaya na mchezaji Hasan Wahabi.

Katika taarifa iliyotolewa na klabu hiyo imeonyeshwa kuhuzunishwa na tukio hilo na kuomba radhi huku ikitaja kuwa tukio hilo halikuwa la kimakusudi.

Imeongeza kuwa, JKT inamuombea kwa Mungu Pacome aweze kupona majeraha yake haraka ili arejee kwenye majukumu yake.

“Uongozi wa JKT Tanzania FC, umehuzunishwa na tukio la kuumia kwa mchezaji wa Yanga SC, Pacome Zouzoua aliyeumizwa na mchezaji Hassan Wahabi, wakati wakiwania mpira, katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, JKT Tanzania FC Vs Yanga SC, uliochezwa katika uwanja wa Major General Isamuhyo, 30 June 2025”.

“Kwa niaba ya mchezaji wa timu ya JKT Tanzania FC, Hassan Wahabi, uongozi tunaomba radhi kwa tukio hilo, ambalo halikuwa la kimakusudi, lililomsababishia maumivu makali Pacome Zouzoua, linalomtesa na kumuumiza kifikra mchezaji wetu Wahabi, kutokana na maumivu aliyoyapata Zouzoua, ambayo hakuyakusudia wala kuyatarajia”.

“Aidha, uongozi wa JKT Tanzania FC, tunatoa pole ya dhati kwa mchezaji Zouzoua, tunamuombea kwa mwenyezi Mungu, apone haraka na arejea katika hali yake ya kawaida, acheze mpira katika kiwango na ubora wake wa siku zote”.

Mexico Yatangulia 16 Bora, Ikiisubiri England u DR Congo