Steve Barker: Msimu Ujao ni Wakati wa Kuvuna Mataji Simba SC
KOCHA Mkuu wa Simba, Steve Barker, amesema anajivunia kiwango cha kujituma kilichoonyeshwa na wachezaji wake katika msimu mzima wa 2025/26, akisisitiza kuwa licha ya kushindwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, kikosi chake kilipambana kwa moyo wote hadi dakika ya mwisho.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa msimu, Barker alisema Simba iliingia katika mchezo wake wa mwisho ikiwa na hamasa na ari ileile ya kutafuta ushindi kama ilivyokuwa tangu mwanzo wa msimu.
Amewapongeza wachezaji wake kwa kupambana bila kukata tamaa katika kila mechi waliyoicheza.
Kocha huyo alitumia nafasi hiyo kuwashukuru viongozi wa klabu, benchi la ufundi, wachezaji na mashabiki wa Simba kwa sapoti, upendo na kujitoa kwao katika kipindi chote cha msimu, akieleza kuwa mchango wao umekuwa wa kipekee kwake.
“Nataka kuishukuru klabu, wachezaji wangu, benchi la ufundi na zaidi mashabiki wa klabu hii kubwa kwa muda, juhudi na ari mliyoonyesha msimu huu. Nyote mna nafasi ya kipekee katika maisha yangu,” amesema Barker.
Barker amesema anafurahishwa na maendeleo ambayo timu imepiga ndani ya miezi sita tangu alipochukua mikoba ya kuinoa Simba, akiamini msingi uliowekwa utaiwezesha timu hiyo kuwa imara zaidi na kufanya vizuri katika misimu ijayo.
Amesisitiza kuwa safari ya mafanikio bado haijaisha, huku akiahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii pamoja na kikosi chake ili kuijenga Simba yenye ushindani mkubwa zaidi katika mashindano ya ndani na kimataifa.
Simba ilihitimisha msimu wa 2025/26 ikiwa katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara na sasa imeanza kuelekeza nguvu katika maandalizi ya msimu mpya kwa lengo la kurejea kwa nguvu na kupigania mataji yote itakayoshiriki.
@@@@Msingi Umewekwa, msimu ujao ni wakati wa kuvuna Mataji; asema kocha Simba