Uncategorized

KOBE BYRANT AZIKWA KWA SIRI

admin February 12, 2020 12:26 pm


VYOMBO mbalimbali vya habari nchini Marekani vimethibitisha kuwa Mchezaji maarufu wa Mpira wa Kikapu, Kobe Byrant (41) na mwanaye, Gianna Maria-Onore Bryant ‘Gigi’ (13) wamezikwa kwa siri Februari 7, 2020, katika Makaburi ya Pacific View Memorial Park, eneo la Corona del Mar mjini California ( kulingana na cheti cha kifo) ikiwa ni wiki mbili tangu vifo vyao vitokee.

Kobe, Gigi na watu wengine saba walipoteza maisha katika ajali ya helikopta iliyotokea Januari 26 katika eneo la Calabasas, California. Walikuwa wakielekea kwenye mchezo wa Kikapu.

Inaelezwa kuwa mazishi hayo ambayo awali yalipangwa kufanyika katika Makaburi ya Westwood Village Memorial Park kabla ya kubadilishwa, yalihudhuriwa na wanafamilia pekee pamoja na watu wachache wa karibu wa familia ya Kobe.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mke wa Kobe, Vanessa Bryant amethibitisha kuwa maombolezo ya pamoja ya vifo vya mumewe na mtoto wake yatafanyika Februari 24 katika Uwanja wa Staples Center.

JOHN BOCCO BALAA LAKE MBELE YA MTIBWA LILIKUWA NAMNA HII HIVI NDIVYO MKAZI WA MBEYA ALIVYOSHINDA ZAIDI YA MILIONI 125 ZA PREMIER BET

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply