Home Uncategorized YANGA YAIVUTIA KASI POLISI TANZANIA

YANGA YAIVUTIA KASI POLISI TANZANIA

BAADA ya kulazimisha sare ya bila kufungana na Tanzania Prisons jana, Februari 15 Uwanja wa Taifa Yanga imeiwahi Polisi Tanzania ya Moshi kwa ajili ya mchezo wa ligi utakaochezwa Februari 18 Uwanja wa Ushirika Moshi.

Yanga ina kumbukumbu ya kulazimisha sare ya kufungana mabao 3-3 kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Uhuru.

Mchezo huo pia ilifungwa hattrick ya kwanza ndani ya ligi kwa msimu wa mwaka 2019/20 na mtupiaji alikuwa ni itram Nchimbi kwa sasa yupo ndani ya Yanga.

Polisi Tanzania itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 3-2 mbele ya KMC kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru.

Nahodha Msaidizi wa Yanga, Juma Abdul amesema kuwa morali ya wachezaji ni kubwa wanahitaji sapoti ya mashabiki ili kufikia malengo.

SOMA NA HII  YANGA YAMTEMESHA BUNGO KOCHA MADEAMA