UONGOZI wa Yanga umewataka mashabiki wao kutokata tamaa kwa timu yao kutokana na kulazimisha sare mbili kwenye mechi zao za Ligi Kuu Bara.
Februari 11, Yanga ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Mbeya City ikalizimisha pia sare ya bila kufungana na Tanzania Prisons mechi zote zilichezwa Uwanja wa Taifa.
Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa mashabiki wanapaswa waelewe kwamba mpira ni mchezo wenye matokeo matatu na unahitaji uvumilivu bila kukakata tamaa.
“Prisons tumewafunga kwenye mechi mbili za hivi karibuni kwao isingekuwa rahisi kukubali tuwafunge tena ndio maana tukashindwa kushinda ila haina maana kwamba tunapaswa kukata tamaa, mashabiki ni wakati wa kuendleea kuisapoti Yanga.
“Bado ligi inaendelea na kuna mechi nyngi za kucheza tutatumia nafasi hiyo kupata ushindi, kikubwa sapoti bila kukata tamaa,” amesema.
Yanga imecheza jumla ya mechi 20 ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi zake 39.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.