UONGOZI wa Yanga umesema kuwa matokeo ya sare mfululizo waliyoyapa yamewafumbua macho na kuwafanya watambue kwamba ligi ya msimu huu wa 2019/20 ni ngumu wanapaswa wajipange zaidi.
Jana Februari 18, Yanga ilipata sare yake ya tatu mfululizo ndani ya Ligi Kuu Bara.
Ilianza kupata sare ya kwanza mbele ya Mbeya City kwa kufungana bao 1-1 na ikafuatia mbele ya Tanzania Prisons bila kufungana na zote ilikuwa Uwanja wa Taifa kisha sare ya tatu ikawa mbele ya Polisi Tanzania Uwanja wa Ushirika kwa kufungana bao 1-1.
Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa wamejifunza kwamba ligi ya msimu huu sio nyepesi.
“Sare ambazo tunazipata kwa msimu huu zikiwa ni mfululizo zinatupa darasa tujue kwamba ligi sio nyepesi nasi tunayapokea ingawa kishingo upande na tunapata picha kwamba timu nyingi zinapambana zikikutana na Yanga,”.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.