Uncategorized

YANGA WAJIPA MATUMAINI YA KUREJEA KWENYE UBORA WAO TENA

admin February 20, 2020 4:22 pm


NAHODHA wa Yanga, Papy Tshishimbi amesema kuwa bado wana nafasi ya kurekebisha makosa yao waliyoyafanya ndani ya Ligi Kuu Bara kwa kupata sare tatu mfululizo.

Yanga inajiaanda na mchezo wake wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union utakaochezwa Februari 23 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Kwenye mechi zake tatu za hivi karibuni imeambulia sare kwa kuanza na Mbeya City kwa kufungana bao 1-1 kisha Tanzania Prisons bila kufunga zote Uwanja wa Taifa ilifunga hesabu mbele ya Polisi Tanzania kwa kufungana bao 1-1.

Tshishimbi amesema:’ Ni matokeo ambayo hatujayafurahia kwani tunaingia uwanjani kutafuta ushindi na kutokana na ushindani kila timu nayo inatafuta ushindi mwisho wa siku tunaambulia sare.

“Bado tuna nafasi ya kurejea kwenye nafasi yetu ya kupata matokeo, benchi la ufundi limeona makosa yetu na litayafanyia kazi,”. 

MZUNGU WA SIMBA ATAKA MABAO MENGI KWA WASHAMBULIAJI WAKE KUPATA POINTI TATU KINACHOWAKOSESHA NGUVU KIPINDI CHA PILI WACHEZAJI WA NAMUNGO HIKI HAPA, DAWA YA AZAM YAANDALIWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply