Home Uncategorized MTIBWA SUGAR:: VIWANJA NI TATIZO,VIBORESHWE

MTIBWA SUGAR:: VIWANJA NI TATIZO,VIBORESHWE


KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila  amesema kuwa kuna umuhimu wa sehemu za kuchezea kuboreshwa ili timu zicheze kwa kujiamini zikiwa ndani ya uwanja.

Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 14 ikiwa imecheza mechi 23 kibindoni ina pointi 24 mchezo wake uliopita ililazimsha sare ya bila kufungana na Tanzania Prisons Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

“Kuna umuhimu wa kufanya maboresho kwenye sehemu za kuchezea ili wachezaji wawe huru kwenye kutafuta matokeo ndani ya uwanja.

“Mechi zetu nyingi tunakwama kushinda kutokana na ubovu wa sehemu za kuchezea jambo ambalo linatugharimu,” amesema.

SOMA NA HII  BAKARI MWAMNYETO ATAJA VIPAUMBELE VYAKE ILI ASAINI