Uncategorized

SIMBA MACHO YOTE KWA KMC, KESHO TAIFA HAPATOSHI

admin February 29, 2020 2:18 am
MABINGWA watetezi Simba kesho, Machi Mosi watakuwa Uwanja wa Taifa kumenyana na KMC mchezo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na kumbukumbu ya kushinda kwa mabao 2-0 Uwanja wa Uhuru kwenye mchezo wa kwanza msimu huu.
Simba iliyo chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck imetoka kushinda mchezo wao wa Kombe la Shirikisho na kutinga hatua ya robo fainali, inakutana na KMC yenye hasira za kufungashiwa virago na Kagera Sugar kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho.
Sven amesema kuwa amekiandaa kikosi chake kwa utulivu ili kuona kinashinda mbele ya KMC ili kupata pointi tatu muhimu.
“Tumetoka kushinda mchezo wetu wa Kombe la Shirikisho mbele ya Stand United, macho yetu kwa sasa ni kwenye mchezo wetu wa ligi dhidi ya KMC, imani yangu tutapata matokeo chanya yatakayotupa pointi tatu” amesema.
AZAM FC WATIA TIMU MAKAO MAKUU, KESHO KUVAANA NA JKT TANZANIA UJUMBE HUU WA YANGA WATUMWA KWA ALLIANCE, GWAMBINA YAIPA KIBURI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply