Home Uncategorized JUVENTUS HAO SASA ANGA ZA MANCHESTER CITY, YAMTAKA GUARDIOLA

JUVENTUS HAO SASA ANGA ZA MANCHESTER CITY, YAMTAKA GUARDIOLA


IMERIPOTIWA kuwa mabosi wa timu ya Juventus inayoshiriki Serie A wapo kwenye mkakati wa kuipata saini ya Kocha Mkuu wa Manchester City, Pep Guardiola.
Mabosi hao wapo tayari kuvunja benki ilikuipata saini ya kocha huyo ili kuiongoza timu hiyo.
Juve iliyo chini ya Maurizio Sarri inamtazama Guardiola kuwa ni mwenye maono makubwa ambaye anaweza kuifanya timu hiyo kufikia malengo makubwa waliyojiwekea.
Rais wa Juve, Andrea Agnelli amesema kuwa ni jambo gumu kumshawishi Guardiola ila imani yao wakimpata itakuwa ni mafanikio makubwa kwao.
Juve ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa Seria A ikiwa na tofauti ya magoli na vinara Inter Milan zote zina pointi 54 kibindoni baada ya kucheza mechi 23 huku Juve ikiwa na mabao ya kufunga 44 na Inter Milan ikiwa na mabao 48.

SOMA NA HII  MO SALAH APIGA HAT TRICK HUKO ENGLAND WAKATI LIVERPOOL IKIPIGA 4G