Home Uncategorized MCHEZO MZIMA WA SIMBA NA KAGERA SUGAR ULIKUWA NAMNA HII

MCHEZO MZIMA WA SIMBA NA KAGERA SUGAR ULIKUWA NAMNA HII

SIMBA jana uwanja wa Taifa walitoa burudani mbele ya mashabiki wake licha ya kushinda bao 1-0 mbele ya Kagera Sugar.
Kagera Sugar ilicheza kwa kujilinda kipindi cha kwanza na kuifanya safu ya ushambuliaji ya Simba iliyo chini ya Meddie Kagere na nahodha John Bocco aliyekuwa akilindwa na nahodha mwenzake Juma Nyosso wa Kagera Sugar kushindwa kufunga bao ndani ya kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili Simba waliongeza mashambulizi kwa Kagera Sugar dakika ya 59 Bocco alichezewa faulo na mlinda mlango Benedict Tinnoco kwenye 18 na mwamuzi kuamuru ipigwe penalti.
Kagere alizamisha nyavuni bao hilo dakika ya 60 na kufikisha jumla ya mabao 13 kwenye ligi akiwa ni kinara wa utupiaji msimu wa 2019/20 na kufanya Simba waifunge Kagera Sugar nje ndani kwani kwenye mechi ya kwanza Uwanja wa Kaitaba Simba ilishinda mabao 3-0.
Simba inafikisha  pointi 59 kwenye ligi ikiwa nafasi ya kwanza na imefunga mabao 47 ikiwaacha Yanga wakiwa nafasi ya tatu na pointi 40 wametofautiana pointi 19 na Yanga ina mechi mbili mkononi ili kuwafikia Yanga kwani wamecheza jumla ya mechi 21 na Simba imecheza mechi 23.
SOMA NA HII  UONGOZI WA YANGA WATAMBA, YANGA KUFIKA MBALI KULIKO KLABU YEYOTE BONGO