Home Uncategorized NAMUNGO FC YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA MWADUI FC

NAMUNGO FC YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA MWADUI FC


HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo FC amesema kuwa kikosi chake kipo sawa na kinaendelea na maadalizi kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mwadui FC utakaopigwa Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Namungo FC imetoka kuichapa bao 1-0 Singida United imefikisha jumla ya pointi 36 baada ya kucheza mechi 20 ipo nafasi ya nne.

Thiery amesema kuwa :”Kila mechi ni ngumu na wanachotazama ni kupata matokeo mazuri kutokana na ugumu ambao wanakutana nao na anaamini watafanya vizuri.

“Kila mechi kwetu ni muhimu kupata ushindi na kilichobaki kwa sasa ni kuona namna gani ambavyo tunaweza kupata pointi tatu muhimu,”.

SOMA NA HII  CAF YAWAONGEZEA MCHEZAJI YANGA