Home Uncategorized YANGA YAWAITA MASHABIKI WAKE KUIPA SAPOTI MKWAKWANI

YANGA YAWAITA MASHABIKI WAKE KUIPA SAPOTI MKWAKWANI


UONGOZI wa Yanga umewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kesho Mkwakwani kuipa sapoti timu yao.

Yanga itamenyana na Coastal Union kwenye mchezo wa pili wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Februari 23, Tanga.

Charles Mkwasa, Kocha Msaidizi wa Yanga, amesema wanatambua mchezo utakuwa na ushindani mkubwa ila hilo haliwapi hofu wapo tayari.

“Mchezo utakuwa mgumu hilo lipo wazi kikubwa tunawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti,”.

SOMA NA HII  MASHINE MPYA 10 ZA DODOMA FC HIZI HAPA